http://jamiiproduction.com/ http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

Wadau wa facebook

Maelezo

Kwa matukio na matangazo wasiliana nasi Simu no' {301}728-3977. Email:swahilivilla@gmail.com

Thursday, April 17, 2014

Angalia Video za Kamati ya Maridhiano Six April 16 2014

Ukawa wasusia Bunge

Dodoma. Mambo yamebadilika. Ukimya ulitawala jana katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge zaidi ya 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia vikao vya Bunge hilo.

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Prof Ibrahimu Lipumba akizungumza katika kikao cha bunge jana ambapo alitangaza kujitoa kwa baadhi ya wajumbe kuendea na mchakato wa kupitisha Rasimu ya Katiba, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Ilikuwa ni saa 10:31 jioni baada ya Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipohitimisha uchangiaji wake akisema: “Ukawa hatuwezi kuendelea kushiriki dhuluma dhidi ya wananchi kwa kupitisha Katiba ambayo ni kinyume cha matakwa yao.”

Baada ya kauli hiyo aliondoka akifuatiwa na Mwenyekiti wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na wajumbe wao kutoka nje ya Bunge.

Ukimya ulitawala takriban dakika mbili hivi na baada ya wajumbe hao kutoka, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samia Suluhu Hassan aliwaelekeza makatibu kuhesabu wajumbe ili kuona kama akidi imetimia ili waendelee na kikao.

Baadaye aliliambia Bunge kuwa makatibu wamemweleza hawahitaji akidi kwa kuwa kikao kilikuwa kinaendelea wakati Ukawa walipotoka nje ya ukumbi.

Boko Haram lawateka nyara wanafunzi 100 Nigeria

Wanamgambo wa kundi la Boko Haram wameshambulia shule ya wasichana ya bweni na kuwachukua mateka zaidi ya wanafunzi 100 kati ya 250 katika mji wa Chibok ulioko katika jimbo la Borno kaskazini mwa Nigeria.

Taarifa zinasema kuwa, shambulizi hilo limefanyika siku mbili baada ya mlipuko wa bomu ambao ulisababisha vifo vya makumi ya watu na kujeruhi wengine wengi pambizoni mwa Abuja, mji mkuu wa Nigeria.

Wanamgambo wa kundi la Boko Haram wamewachukua mateka wanafunzi hao wasichana wa shule ya serikali kwenye lori moja na kutokomea nao mahala pasipojulikana. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, shambulio hilo lilidumu kwa muda wa masaa sita, bila ya kupatikana usaidizi wowote wa jeshi la polisi.

Taarifa hizo zinasema kuwa, wanamgambo hao walishambulia pia eneo moja lililoko karibu na shule hiyo na kufanya uharibifu mkubwa wa nyumba na mali za wakazi wa eneo hilo.

Kamishna wa Polisi katika jimbo la Borno amethibitisha kutokea utekwaji nyara wanafunzi hao wasichana wa shule ya bweni wenye umri wa kati ya miaka 16 na 18.

Heartbreaking aerial images show bodies of elephants slaughtered by vicious poachers lying in the Kenyan wilderness

These heartbreaking images show the carcasses of 11 elephants discarded in a Kenyan wildlife reserve after poachers killed them for their ivory tusks.

The distressing photos highlight how poaching is still rife across the Tsavo Conservation Area which is one of Kenya's oldest strongholds for elephants.

The aerial images were taken in January by members of the David Sheldrick Wildlife Trust (DSWT) who patrol the area daily to try and protect the habitat and the animals living there.

Distressing: This heartbreaking image shows four of the 11 elephants hunted down and killed by poachers in the Tsavo Conservation Area in Kenya in January
Distressing: This heartbreaking image shows four of the 11 elephants hunted down and killed by poachers in the Tsavo Conservation Area in Kenya in January

Hunted: A carcass of an elephant killed by poachers in a Kenyan wildlife reserve. Poaching is still rife across the region
Hunted: A carcass of an elephant killed by poachers in a Kenyan wildlife reserve. Poaching is still rife across the region

Reserve: Elephant herds are pictured making their way through dense vegetation in Nairobi National Park
Reserve: Elephant herds are pictured making their way through dense vegetation in Nairobi National Park

Tsavo National Park is home to Kenya's largest population of elephants which now number some 12,000.

The population was decimated by poachers during the 1970's and 1980's but their numbers have been steadily increasingly following the introduction of the DSWT's elephant Reintegration Centre.

Sourece: dailymail.co.uk

Wednesday, April 16, 2014

Sikiliza kwa makini Sauti ya VIMBWANGA vya Profesa Lipumba kabla UKAWA hawajatoka Bungeni

Mchango wa Zitto Kabwe kuhusu Sura ya 1 na 6 ya Rasimu ya Katiba

Ufuatao ni mchango alioutoa Mhe. Zitto Kabwe katika kikao cha leo APrili 16, 2014 cha Bunge Maalum na Katiba kilichopokea maoni ya Wajumbe kuhusu rasimu tajwa hapo juu.

Ndugu Mwenyekiti,

Kamati 12 za Bunge lako tukufu zimeleta Taarifa zake mbele yetu kwa ajili ya maboresho ya Rasimu ya Katiba ili kupata katiba inayopendekezwa itakayopelekwa kwa Wananchi. Maoni ya Kamati yamegawanyika katika aina Kuu 2, maoni ya walio wengi na maoni ya walio wachache. Ndani ya Bunge hili majadiliano pia yamekuwa yenye mwelekeo huo huo na kwa kweli hakuna majadiliano bali majibizano. Sio afya kwa nchi yetu hata kidogo kuwa na Taifa ambalo wawakilishi wake kwenye Baraza nyeti kabisa kama hili wanajibizana badala ya kujadiliana, wanabishana badala ya kuongea na wanatukanana badala ya kushawishiana.

Imefikia hatua zinatoka lugha za kibaguzi bila kukemeana na badala yake tunashangiliana na kupigiana vigelegele. Ubaguzi wa rangi au ubaguzi wa aina yeyote ile ni sumu kali dhidi ya umoja wetu na Utu wetu. Kauli za kibaguzi, matusi dhidi ya waasisi na dhidi yetu wenyewe ni mambo ya kulaani kwa ukali unaostahili.

Ni muhimu kutambua kuwa tofauti na mabadiliko ya katiba yaliyowahi kufanyika nchini, mchakato huu wa sasa ni wa kipekee ambao unatoa nafasi kwa watanzania wote wa makundi yote kushiriki kwa njia moja ama nyingine. Ni wajibu wetu kutambua kuwa kuwa huu ni mchakato shirikishi ambao umelenga kuleta maridhiano ya makundi yote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi na sio kuongeza mgawanyiko uliopo katika jamii yetu. Endapo tutafanikiwa kuendesha mchakato huu katika hali ya kuheshimiana, kuthaminiana na kwa nia njema sio tu tutaweza kujenga mwanzo mpya wa kisiasa wenye kujali umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa lakini pia tutaweza kuerejesha imani yao kwa dola, serikali, viongozi na wanasiasa, imani ambayo imekuwa ikitoweka na hata kuathiri uhalali wa dola letu mbele ya macho na mioyo ya watanzania na kutishia hatma ya taifa letu. Mwenendo wa mchakato huu una umuhimu wa kipekee kulinusru taifa letu kutoka kwenye dalili mbaya tunazoziona kila siku zikijongea utaifa wetu.

UN inatiwa hofu na hali ya raia wa Sudan Kusini walioko ukimbizini

Wakimbizi wa ndani kutoka Sudani Kusini  wakipewa hifadhi katika kambi ilyojengwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Khor Abeche.
Wakimbizi wa ndani kutoka Sudani Kusini 
wakipewa hifadhi katika kambi ilyojengwa 
kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa 
mjini Khor Abeche.
REUTERS/Albert Gonzalez Farran
Na RFI

Zaidi ya wakimbizi elfu moja toka nchi ya Sudan Kusini wanaingia nchini Ethiopia kila siku, huku wengi wao wakikabiliwa na hali mbaya na wako hatarini kupoteza maisha, na hii ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa UN.

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake linaloshughulikia wakimbizi duniani UNHCR, unasema kuwa karibu asilimia 95 ya wakimbizi wanaoingia nchini humo wengi ni wanawake na watoto na kuongeza kuwa wengi walikuwa wakitumikishwa kwenye makundi ya wapiganaji nchini Sudan Kusini.

UNHCR inasema kuwa iwapo raia hao hawatapata msaada wa haraka, hali itakuwa mbaya zaidi na pengine kushuhudia vifo wakati huu nchi hiyo ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya elfu 95 wa Sudan Kusini.

Zaidi ya raia laki mbili wa Sudan Kusini wameomba hifadhi nchini Sudan, Uganda na Kenya wakati watu laki 8 hawana makaazi ya kudumu ndani ya Sudan Kusini yenyewe.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine zaidi ya 1.000.0000 wameyahama makaazi yao, laki 8 wakiwa ni wakimbizi wa ndani na wengine laki 3 wamekimbilia nje ya nchi.

Tangu machafuko kutokea 15 desemba mwaka 2013, raia wa Sudan Kusini 61.000 wamekimbilia Sudan, 97.000 wamekimbilia nchini Rwanda, 95.700 wamekimbilia nchini Ethiopia na 33.400 wanapewa hifadhi nchini Kenya, wakihofia usalama wao na njaa inayolikabili taifa hilo changa.

MAELEZO YA MHE PIUS NA ALI MZEE ALI WALIPOHOJIWA NA JAMBO TANZANIA

Dubai cost of living rising at highest rate since 2009

By Staff writer | Al Arabiya News, Dubai. Wednesday, 16 April 2014

Rising housing and food prices have pushed Dubai’s inflation rate to the highest since 2009, with the cost of living in March up 3 percent on the year before.

Housing and utility costs were up 4.8 percent in Dubai in March. (File photo: Shutterstock)

Housing and utility costs, which account for almost 44 percent of consumer expenses, were up 4.8 percent, and rose 0.4 percent month-on-month in March, Reuters said, quoting data from the Dubai Statistics Center.

The cost of food and drinks also rose 4.8 percent from a year earlier and gained 1.2 percent from a month earlier.

Inflation is now at the highest level since August 2009, the year the global financial crisis caught up with Dubai and brought state-owned Dubai World and its subsidiary Nakheel to a debt standstill.

Nakala ya saini za hayati A. A. Karume zinazotiliwa mashaka

Baada ya kabrasha linaloonesha 'hati halisi' ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuoneshwa hadharani juzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Ombeni Sefue, baadhi ya wananchi wameonesha wasiwasi na kuhoji ukweli wa halali ya saini inayoonekana katika hati hiyo na saini zilizoko kwenye nyaraka nyingine.

More than 300 people missing after South Korea ferry sinks

More than 300 people were missing after a ferry sank off South Korea, the coastguard said on Wednesday, with a three-fold increase in the number of passengers unaccounted for put down to a miscalculation by officials.

Part of South Korean passenger ship ''Sewol'' that has been sinking is seen as South Korean maritime policemen search for passengers in the sea off Jindo April 16, 2014. Reuters
Part of South Korean passenger ship ''Sewol'' that has been sinking is seen as South Korean maritime policemen search for passengers in the sea off Jindo April 16, 2014. Reuters

The ferry was carrying 477 people, of whom 164 were confirmed rescued, coastguard officials said. Two people were confirmed dead after the ferry listed heavily onto its side and capsized in apparently calm conditions off South Korea’s southwest coast.

The Ministry of Security and Public Administration had reported that 368 people had been rescued and that about 100 were missing.

It later described those figures as a miscalculation, turning what had first appeared to be a largely successful rescue operation into potentially a major disaster.

The cause of the disaster was not immediately clear.

Most of those on board were children and their teachers from a high school in Seoul on a field trip to Jeju island, about 100 km (60 miles) south of the Korean peninsula.

There were 477 people and 150 vehicles on board the ferry Sewol, officials said. Witnesses said many people were likely still inside the stricken vessel.

Waziri wa Uingereza atoa angalizo la gesi

Na Goodluck Eliona, Mwananchi

Dar es Salaam. Tanzania imeshauriwa kutotishwa na migogoro mbalimbali barani Afrika inayotokana na rasilimali za gesi na mafuta, badala yake ifuate mipango yake iliyojiwekea ili kuwanufaisha wananchi wote.

Barker alisema Tanzania ina bahati kupata rasilimali hizo na kwamba zinaweza kubadilisha maisha ya wananchi kwa kuwaletea maendeleo makubwa iwapo tu hawataangalia historia ya migogoro iliyotokana na upatikanaji wa gesi na mafuta kwenye nchi nyingine za Afrika.PICHA|MAKTABA

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi wa Uingereza, Greg Barker katika mahojiano maalumu na mwandishi wetu nyumbani kwa Balozi wa nchi hiyo hapa nchini.

Barker alisema Tanzania ina bahati kupata rasilimali hizo na kwamba zinaweza kubadilisha maisha ya wananchi kwa kuwaletea maendeleo makubwa iwapo tu hawataangalia historia ya migogoro iliyotokana na upatikanaji wa gesi na mafuta kwenye nchi nyingine za Afrika.

Alisema ujio wa gesi nchini utalisaidia taifa kukabiliana na ongezeko la uharibifu wa mazingira kwa kuacha kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuanza kutumia nishati hiyo.

Pia katika ziara hiyo iliyomkutanisha na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge, Barker alitembelea mradi mkubwa wa umeme wa nishati ya upepo huko Singida utakaozalisha megawati 100 unaosimamiwa kwa ubia na Kampuni ya Aldwych ya Uingereza.

Liberia jails Ugandan woman over heroin

A criminal court in the Liberian capital Monrovia on Monday sentenced a 24-year-old Ugandan national, Shirak Nalwadda to four years imprisonment for unlawful possession and distribution of narcotic drugs.

law
Presiding Judge, Blamo Dixon imposed the sentence on Nalwadda after jurors reached a unanimous guilty verdict in less than an hour of deliberation.

Meanwhile, the judge ordered defendant Nalwadda to be deported from Liberia through diplomatic channels with arrangements made for her to serve her sentence in Uganda.

He also ordered that the convict be remanded in custody at the Monrovia Central Prisons pending her deportation to Uganda.

Nalwadda was arrested at the Roberts International Airport on Saturday, November 30,2013 with a parcel containing 1.2 kilograms of heroin.

Its street value was estimated at $30,000.